14 wauawa vitani Yemen

Haki miliki ya picha AFP
Image caption 14 wauawa vitani Yemen

Yamkini watu 14 wameuwawa katika mapigano makali yaliyozuka katika mji wa Aden Kusini mwa Yemen.

Maafa hayo yametokea baada ya majeshi ya serikali yanayokabiliana na wanamgambo wa Islamic State kuutwa tena udhibiti wa mji huo.

Majeshi ya muungano yanayoongozwa na Saudi Arabia yameamua kutumia mashambulizi ya angani dhidi ya makundi ya wapiganaji katika eneo hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Al Qaida na Islamic State, yameanza kutumia mbinu za kuvizia dhidi ya majeshi ya muungano.

Makundi hayo ya waasi, yaliyo na uhusiano mitandao ya al Qaida na Islamic State, yameanza kutumia mbinu za kuvizia dhidi ya majeshi hayo ya muungano.

Makundi hayo mawili ya jihadi yametumia vita kati ya serikali ya Yemen na waasi wa Houthi kupanua maeneo chini ya udhibiti wao katika maeneo ya Kusini na Mashariki mwa Yemen.