Mwanamfalme wa Saudia amkosoa Obama

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwanamfalme wa Saudia amkosoa rais wa Marekani Obama

Mwanamfalme wa cheo cha juu nchini Saudi Arabia, amekosoa vikali madai ya rais wa Marekani Barack Obama kuwa nchi yake haijafanya jitihada kuisaidia Marekani kukabiliana na matatizo yaliyo eneo la mashariki ya kati.

Image caption Mwanamfalme Turki al-Faisal

Kwa njia ya barua ya wazi,Turki al-Faisal , alisema kuwa Saudi Arabia imekuwa kiongozi katika jitihada za kukabilia na kundi la Islamic state.

Mwanamfalme huyo pia amesema kwa Saudi Arabia imetoa habari za kijasusi zilizozuia kutokea mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani.