Oparesheni dhidi ya ugaidi yawageukia polisi Ubelgiji

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Oparesheni dhidi ya Ugaidi nchini Ubelgiji

Vikosi vya maafisa wa usalama nchini Ubelgiji vinawasaka watu wawili baada ya maafisa wa polisi kufyatuliwa risasi katika oparesheni dhidi ya ugaidi katika mji mkuu wa Brussels.

Kisa hicho kilitokea katika makaazi ya kusini ya Forest.Maafisa watatu walijeruhiwa huku mmoja wao akijeruhiwa vibaya.

Mwendesha mashtaka amesema kuwa uvamizi huo unahusishwa na shambulio la Paris ambalo liliwaua watu 130 mwezi Novemba.

Maafisa wa polisi wa Ubelgiji wamekuwa wakijaribu kuwasaka wapiganaji kutoka kwa kundi la Islamic State.

Baada ya kisa cha Jumaane ,maafisa wa polisi wamesema kuwa wanawasaka washukiwa wawili waliotorokea kwenye paa la nyumba.

Eric Van Der Sypt,msemaji wa waendesha mashataka hao waliambia AFP kwamba maafisa wa polisi walifyatuliwa risasi wakati wa shambulio hilo la jumanne mchana.

Ameongezea kuwa msako huo unahusishwa na uchunguzi wa shambulio la Paris.