Bomu lalipuka ndani ya gari Berlin

Haki miliki ya picha
Image caption Bomu mjini Berlin

Maafisa wa polisi mjini Berlin wameanzisha uchunguzi wa mauaji baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka na kumuua dereva.

Mlipuko huo ulitokea wakati gari hilo lilipokuwa likelekea katikati mwa mji huo.

Lililirusha gari hilo hewani kulingana na maafisa.Maafisa wa polisi waliwaambia wakaazi wa eneo hilo kufunga madirisha yao na kukaa nyuma ya nyumba zao.

Lakini kundi la wataalam wa kutibua mabomu limesema kuwa hakuna hatari ya milipuko.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari hilo aina ya Volkswagen Passat wakati ilipokuwa ikisafiri kuelekea Bismarckstrasse wakati wa saa za asubuhi ,msemaji wa polisi alisema.

Msemaji wa afisi ya mwendesha mashtaka amesema kuwa walidhania kwamba mamlaka ilikuwa ikikabiliana na mauaji kulingana na vyombo vya habari vya Ujerumani.

Polisi wanasema uchunguzi wa mauaji unaendelea.