Htin Kyaw ndio rais mpya wa Myanmar

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwandani wa San Suu Kyi ,Htin Kyaw kushoto

Bunge nchini Myanmar limemchagua Htin Kyaw,mwandani wa kiongozi anayependelea demokrasia Aung San Suu Kyi kama rais wa taifa hilo.

Uteuzi huo ndio hatua ya hivi karibuni ya mageuzi baada ya miongo kadhaa ya uongozi wa kijeshi.

Aung San Suu Kyi hawezi kuwa rais wa taifa la Myanmar kulingana na katiba,lakini amesema kuwa atakuwa kama rais.

Htin Kyaw amepongeza ushindi wake kuwa ushindi wa Bi San Suu Kyi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Htin Kyaw

Alisimama dhidi ya wagombea wengine wawili akiwemo jenerali mmoja aliyesimamishwa na jeshi.

Htin Kyaw atachukua mahala pake Thein Sein ambaye amepata sifa kwa kusaidia kuleta demokrasia baada ya miongo kadhaa ya uongozi wa kidikteta wa jeshi.