Koo ndio zinazotoa bima za magari Somalia

Image caption Magari ya Somaliland

Barabara ya Hargeisa,katika mji mkuu wa jimbo lililojitenga la Somaliland zinaendelea kujaa magari

Matumizi ya magari yameongezeka na serikali imeanza mpango wa kuimarisha barabara zake kupitia usaidia wa muungano wa Ulaya.

Kumekuwa na ongezeko la ajali barabarani huku watu 30 wakiuawa kufikia sasa mwaka huu.

''Mojawapo ya ajali kubwa ya mwaka ilisababisha watu 14 kufariki huku wengine wengi wakijeruhiwa'',alisema Abdiwahaab Nakruma kutoka kwa wizara ya afya.

''Waendeshaji wengi wa magari hawana bima ya magari'' .

Kampuni ya kipekee inayotoa bima kwa magari Takaful,ilia BBC kwamba wanafanya kazi na maafisa kutoka serikalini pamoja mashirika ya kimataifa.

Ili kulipa uharibifu wakati wa ajali,watu wengi huelekea katika koo zao.

Mwendeshaji gari Abdi Hussein amesema kuwa wajibu wote hutekelezwa na koo kwa kuwa hakuna bima.

Wakuu wa koo hizo huchukua na kusimamia fedha kupitia mpango unaoitwa MAG.

Image caption Magari ya Somaliland

Mmoja wao Hassan Juma aliambia BBC kwamba kila mmoja hutegemea koo yake ili iwajibike kwa uharibifu na ni jukumu lao kuwalipia wanachama.

Hilo halishangazi.Mpango huo wa kutegemea koo una mizizi katika jimbo la Somaliland,na watu huamini sana koo zao.