Wapiganaji wadhibiti mji wa Somalia

Image caption Maharamia katika pwani ya Somalia

Kundi moja la wapiganaji lililokuwa katika mashua limewasili katika pwani ya jimbo la Somalia Puntland na kuudhibiti mji huo.

Watu sasa wanatorokea Gara'ad alisema Farhaan Farh Abdi.

Shahidi mwengine ambaye hakutaka kutajwa alisema kuwa wapiganaji hao walishusha silaha zao kutoka kwa boti hiyo.

Mji huo ulikuwa kambi kuu ya maharamia ,lakini wapiganaji hao wanadaiwa kutoka katika kundi la kigaidi la al-shabab.

''Waliwasili kwa maboti makubwa na kuyateka nyara maboti ya wavuvi bwana'', Abdi alisema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alshabab

Siku ya Jumatatu ,kundi jingine la wapiganaji wa al-shabab liliingia katika eneo la Gara'ad na kulala katika eneo hilo.

Kuna ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba kundi hilo baadaye liliondoka kwa kutumia barabara baada ya wenzao kuwasili na kuudhibiti mji huo.