Majimbo 5 kuwateua wagombea urais Marekani

Image caption Wagombea wa urais nchini Marekani

Majimbo matano nchini Marekani yanapiga kura kumteua mgombea atakayewania urais kupitia tiketi ya vyama vyao.

Uchaguzi huo huenda ukawapa fursa wagombea wa vyama vya Democrat na Republican kuimarisha uongozi wao.

Kura zimeanza kupigwa katika jimbo la Ohio na Florida yote yakionekana kuwa muhimu pamoja na majimbo ya Carolina Kaskazini ,illinois na Missouri.

Mgombea wa chama cha Democratic aliye kifua mbele Hillary Clinton atatumai kwamba atafanikiwa kum'bwaga mpinzani wake wa karibu Bernie Sanders .

Haki miliki ya picha
Image caption Raia wapiga kura

Wakati huohuo Donald Trump atalenga kuwaangusha wapinzani wake katika kinyang'anyiro hicho.

Bilionea huyo anapigiwa upatu kushinda uteuzi wa mgombea wa Republican lakini anakabiliwa na upinzani katika chama cha Republican pamoja na chama cha Democrats.

Aliandikisha ushindi wa mapema siku ya jumapili wakati aliposhinda wajumbe wote tisa katika kisiwa cha Kaskazini cha Mariana.