Argentina yaizamisha meli ya Uchina

Haki miliki ya picha Prefectura Naval Argentina
Image caption Meli ya China iliozamishwa na walinzi wa pwani ya Argentina

Walinzi wa pwani nchini Argentina wamesema kuwa wameifukuza na kuizamisha boti moja ya Uchina iliokuwa ikivua samaki kinyume cha sheria katika maji ya taifa hilo siku ya Jumatatu.

Katika taarifa ,walinzi hao wa pwani wamesema kuwa mojawapo ya boti hizo iliionya boti hiyo ya Lu Yan Yuan Yu 010 kwa kuifyatulia risasi iliopukwa ikielekea katika maji ya kimataifa.

Walinzi hao wanasema kwamba waliionya kupitia kipaza sauti.

Wafanyikazi wote 32 wa boti hiyo waliokolewa.

Uchina imeonyesha wasiwasi wake kuhusu kuzamishwa kwa boti hiyo.

Msemaji wa wizara ya kigeni wa taifa hilo Lu Kang alisema katika taarifa kwamba Beijing imewasilisha wawakilishi wake nchini Argentina ikitaka uchunguzi kamili kufanywa kuhusiana na kisa hicho.

Uvuvi haramu ni tatizo la kawaida katika eneo hilo.

Mara nyingi boti zinazopatikana zikifanya uovu huo hutafuta mbinu za kugongana na walinzi hao na hivyobasi kuhatarisha sio maisha ya wafanyikazi wake bali hata yale ya walinzi hao wa pwani,ambao waliamrishwa kuifyatulia risasi meli hiyo,taarifa hiyo ya walinzi wa pwani hiyo walizungumza kwa lugha ya kihispania.

Hatua hiyo inajiri licha ya uhusiano wa Argentina na Uchina kuimarika katika siku za hivi karibuni.