Kiraithe ateuliwa msemaji wa serikali Kenya

Kiraithe
Image caption Bw Kiraithe amekuwa mkuu wa usalama viwanja wa ndege Kenya

Msemaji wa zamani wa polisi Kenya Eric Kiraithe ameteuliwa kuwa msemaji wa serikali ya taifa, ambao ni wadhifa mpya serikalini.

Bw Kiraithe amekuwa akihudumu kama meneja wa usalama wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya.

Taarifa kutoka ikulu imesema Bw Kiraithe atakuwa akihudumu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa ambayo ndiye pia inayosimamia masuala ya usalama.

Bw Manoah Esipisu anasalia kuwa msemaji wa ikulu na ataendelea kuhudumu kutoka kwa Afisi ya Rais.

Mkuu mpya wa utumishi wa umma Bw Nzioka Waita, kupitia taarifa, amesema mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha uhmawasiliano kati ya serikali na umma kuhusu ajenda ya serikali ya kitaifa.