Waandamana dhidi ya uteuzi wa Lula Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano Brazil

Raia wa Brazil nchini Sudan Kusini wamefanya maandamano katika miji kadhaa wakipinga hatua ya rais Dilma Rousseff ya kumteua mtangulizi wake Luiz Inacio Lula da Silva kama mkuu wa wafanyikazi.

Katika mji mkuu wa Brasilia ,maafisa wa polisi waliwarushia waandamanaji maji yenye pilipili nje ya jumba la rais.

Lula anachunguzwa katika kashfa kubwa ya ufisadi.Saa chache baada ya hatua hiyo ,jaji wa kijimbo anayeongoza uchunguzi dhidi ya Lula alitoa mawasiliano ya simu yaliorekodiwa yakionyesha kwamba bi Lula alimpatia wadhfa huo ili kumkinga dhidi ya kukamatwa.

Kiongozi huyo wa Brazil ambaye yeye mwenyewe anakabiliwa na mashtaka alitetea uteuzi huo.Amesema kuwa Lula ana ujuzi mkubwa kama mpatanishi wa kisiasa ambaye atasaidi kuupiga jeki uchumi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamana dhidi ya uteuzi wa Lula da silva

Pia alisema kuwa rais huyo wa zamani anaweza kushtakiwa na mahakama ya juu.

Sauti hiyo ya mawasiliano ilizua hisia kali katika bunge la Brazil huku kukiwa na visa vya ghasia baada ya viongozi wa upinzani kumtaka rais huyo kujiuzulu.