Wapiganaji 30 wa al-Shabab wauawa Puntland

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Kenya

Takriban washukiwa 30 wa kundi la wapiganaji wa al-shabab wameuawa katika makabiliano ya maeneo mawili tofauti na vikosi vya Somalia pamoja na vile vya Kenya.

Mamlaka ya jimbo lililojitenga la Puntland wanasema kuwa wapiganaji 11 wa Islamic State waliuawa wakati walipojaribu kuviteka vijiji kadhaa vya pwani ya Kenya.

Jeshi la Kenya limesema kuwa liliwauawa wapiganaji 19 ambao walishambulia kambi moja ya kijeshi katika mji uliopo kusini mwa Somalia wa Afmadhow.

Wapiganaji wa Al-shabab hawajatoa tamko lao kuhusu kisa hicho ambacho kilitokea siku ya Jumatano.