Kundi la Kikurdi lakiri kutekeleza mauaji Uturuki

Image caption Shambulio la kigaidi mjini Ankara Uturuki lililosababisha vifo vya watu 37

Kundi la wanamgambo wa Kikurdi TAK limekiri kutekeleza shambulizi baya zaidi siku ya jumapili katika mji mkuu wa Ankara.

Katika taarifa iliotumwa mitandaoni,shambulio hilo lililowauwa watu 37 lilikuwa la kulipiza kisasi oparesheni za kijeshi katika eneo la wakurdi la Kusini Mashariki.

TAK ambalo ni chimbuko la kundi lililopigwa marufuku la chama cha wafanyikazi wa Kikurdi PKK tayari limekiri kutekeleza shambulio jingine mjini Ankara mwezi uliopita.

Mamlaka ya Uturuki imelaumu PKK kwa kutekeleza shambulio hilo.

Wakati huohuo Ujerumani imefunga ubalozi wake mjini Ankara pamoja na shule moja mjini Instabul siku ya Alhamisi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndugu na marafiki za waathiriwa wa mlipuko nchini Uturuki

Waziri wa maswala ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema kuwa kuna ushahidi kwamba wapiganaji walikuwa wakijitayarisha kushambulia maeneo manne nchini Uturuki.

Watalii 12 wa Ujerumani waliuawa katika shambulio la kujitolea muhanga linalodaiwa kutekelezwa na wapiganji wa IS mjini Istanbul mnamo mwezi Januari.