Maandamano dhidi ya serikali yafanyika Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano Brazil dhidi ya serikali

Polisi nchini Brazil wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwazuia waandamanaji kutoka kwa makaoa makuu ya rais Dilma Roussef.

Maelfu ya watu wanaotaka ajiuzuli waliandamana katika mji mkuu Brasilia.

Wanamlaumu rais Roussef na chama chake cha workers party kwa ufisadi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Dilma Rousseff na Lula da Silva

Pia kulikuwa na maandamano ya kumpinga Roussef katika mji mkubwa zaidi nchini Brazil wa Sao Paolo.