Arsenal yailaza Everton

Image caption Arsenal dhidi ya Everton

Arsenal ilijibu kuondolewa kwake katika kombe la vilabu bingwa Ulaya pamoja na lile la FA baada ya kuishinda Everton katika uwanja wao wa Goodison Park.

Danny Welbeck aliiweka kifua mbele Arsenal baada ya kufunga katika dakika ya saba ya kipindi cha kwanza baada ya kupata pasi kutoka kwa Sancheza na kumchenga goli kabla ya kufunga.

Katika dakika ya 42 Kijana Alexi Iwobi aliwafurahisha mashabiki wa Arsenal baada yankufunga bao lake la kwanza katika kilabu hiyo.

Image caption Arsenal dhidi ya Everton

Matokeo hayo yanaiweka Arsenal pointi nane nyuma ya viongozi wa ligi Leicester City.

Ni ushindi wa kwanza wa Arsenal katika mechi nne za ligi ya Uingereza.

Everton ilishambulia mara mbili pekee katika lango la Arsenal.