Mahakama yamzuia Lula kuchukua wadhfa Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa rais wa Brazil Lula da Silva

Mahakama ya juu zaidi nchini Brazil imemzuia rais wa zamani Luis Inacio Lula da Silva kuteuliwa kuwa mkuu wa utumishi wa umma.

Uamuzi huo sasa unairudisha kesi dhidi yake kuhusu ulanguzi wa pesa mahakamani .

Kumekuwa na hatua za kisheria kukabiliana na kuteuliwa kwake katokana na madai kuwa alikuwa akilindwa kutokana na uchunguzi wa kuhusika kwenye ufisadi.

Uamuzi wa hivi punde unatolewa muda mfupi baada ya Lula kuhutubia maelfu ya watu katika mkutano wa kuiunga mkono serikali mjini Sao Paulo.