Kanda ya ngono: Mahakama yamlipa Hulk Hogan $115m

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hulk Hogan akishiriki mieleka

Jopo la waamuzi mjini Florida limempatia aliyekuwa nyota wa mchezo wa mieleka Hulk Hogan kitita cha dola milioni 115 kama malipo baada ya mtandao mmoja wa udaku Gawker kuchapisha kanda moja ya ngono ya mchezaji huyo ambaye amestaafu.

Mawakili wa Bwana Hogan walihoji kwamba mtandao huo wenye makao yake huko New York ulikiuka haki za faragha za Hogan na kwamba kanda hiyo ilikuwa haina habari mpya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hulk Hogan

Kesi hiyo iliokuwa na makabiliano kati ya uhuru wa vyombo vya habari dhidi ya haki ya faragha ya mtu maarufu ilifuatiliwa kwa karibu.

Kanda hiyo ya video ilichapishwa mwaka 2012 baada ya Hogan kurekodiwa akifanya ngono na mke wa rafikiye.

Mawakili wa Gawker walihoji kwamba ijapokuwa jopo la waamuzi huenda ukavichukia vitendo vya mtandao huo,swala la uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu sana.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mahakamani

Wakili wa Bwana Hogan alisema kuwa Gawker haikuwasiliana naye wala mwanamke aliyekuwa katika kanda hiyo kabla ya kuichapisha.