Mitt Romney:Cruz ndiye atakayemzuia Trump

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mitt Romney

Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani Mitt Romney amesema kuwa atampigia kura seneta wa Texas Ted Cruz kwa kuwa ''havutiwi'' na mgombea wa chama hicho aliye kifua mbele Donald Trump.

Bwana Romney amesema katika mtandao wake wa facebook kwamba njia ya kipekee ya kumchagua mgombea wa Republican ni kupitia mkutano ambapo wanachama wanamchagua atakayegombea kupitia chama hicho.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Donald Trump na Mitt Romney

Alifanya kampeni na Gavana John Kasich huko Ohio lakini akasema kuwa kumpigia kura Bwana Cruz ndio nijia ya kipekee kumzuia Trump.

Anajiunga na viongozi wengine wa Republican wanaomuunga mkono Bwana Cruz.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ted Cruz

Bwana Trump ameshinda majimbo mengi na kwa sasa ana takriban wajumbe 678 huku akitakiwa kujipatia wajumbe 1237 kushinda uteuzi huo.