Upigaji kura waendelea Congo Brazzaville

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Denis Sassou Nguesso amekuwa madarakani kwa miaka 32

Upigaji kura unaendelea nchini Congo Brazzaville ambapo wapiga kura wanamchagua rais mpya kutoka kwa wagombea tisa.

Rais wa sasa Denis Sassou Nguesso ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 32 anagombea urais kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Utawala umeamrisha makampuni mawili makubwa zaidi ya mawasiliano kufunga mifumo yote ya mawasiliano leo Jumapili na Jumatatu kutoka na sababu za kiusalama.

Mapema leo, upigaji simu kwenda Congo haukufanikiwa. Waziri wa mawasiliano nchini humo Thierry Moungalla aliiambia BBC kuwa hatua hiyo ilichukuliwa ili kuuzuia upinzani usichapishe matokeo yake vile ulivyohaidi wakati wa kampeni.