Mwandishi wa DW aliyetoweka apatikana

Salma Haki miliki ya picha DW Facebook
Image caption Salma alikamatwa na watu wasiojulikana Ijumaa

Mwandishi aliyewakilisha kituo cha redio cha Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) visiwani Zanzibar Salma Said na ambaye alitoweka Ijumaa, amepatikana.

Kamanda wa polisi wa Dar es Salaam Simon Siro amethibitisha kupatikana kwa mwanahabari huyo.

BBC imezungumza na Mume wa Salma Said, Bw Ali Salim Khamis, ambaye amesema kwa sasa Salma anatoa maelezo kwa polisi Dar es Salaam.

Bi Said alikuwa pia mwandhishi wa magazeti ya Mwananchi Communications.

Idhaa ya DW baadaye iliandika kwenye Facebook kwamba mwandishi huyo alipatikana jijini Dar es Salaam.