Moja kwa Moja: Kura zahesabiwa Zanzibar

Bofya hapa kwa habari kuhusu matokeo

20:50 Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetoa picha za baadhi ya viongozi wa Zanzibar wakipiga kura leo. Miongoni mwao ni Mke wa Rais Mstaafu wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume.

Haki miliki ya picha ZEC

20:30 Matokeo yanapoendelea kusubiriwa, baadhi ya waangalizi wamezungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi wa marudio ulivyofanyika.

Huwezi kusikiliza tena

17:40 Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Wilaya ya Mjini Magharibi Bw Mohammed Ali Abdallah amesema uchaguzi umekamilika salama. Amewasihi wakazi wa visiwani wakubali matokeo yatakayotoka vituoni na wadumishe amani na utulivu.

17:27 Maafisa wa usalama wanashika doria vituoni. Hapa ni kituo cha shule ya upili ya Ben Bella.

17:21 Shughuli ya kuhesabu kura kituo cha shule ya sekondari ya Ben Bella inaendelea. Tazama video hii fupi kuhusu uhesabu wa kura.

Huwezi kusikiliza tena

16:32 Kura zimeanza kuhesabiwa katika vituo mbalimbali. Kwenye picha hapa chini, kura zinahesabiwa katika kituo cha shule ya upili ya Ben Bella.

16:24 Katika kituo cha shule ya upili ya Ben Bella, shughuli ya upigaji kura imekamilika, masanduku yakafunguliwa na karatasi za kura zikaanza kupangwa tayari kuanza kuhesabiwa.

Image caption Karatasi za kura zikipangwa Ben Bella
Image caption Karatasi za kura zikimwagwa Ben Bella
Image caption Masanduku ya kura baada ya shughuli kukamilika shule ya upili ya Ben Bella

16:00 Vituo vya kupiga kura sasa vyafaa kufungwa rasmi. Wapiga kura walio vituoni hata hivyo wanaruhusiwa kupiga kura hadi saa kumbi na mbili jioni.

15:50 Vituo vya kupigia kura vinafaa kufungwa saa kumi. Katika kituo cha Madungu, Pemba hakuna wapiga kura waliosalia. Watu pekee ni maafisa wa usalama, maafisa wa tume na mawakala wa vyama.

15:30 Mwandishi wa BBC aliyeko Pemba Arnold Kayanda anasema wakazi wametumiwa ujumbe wa SMS wa kuwasihi wakapige kura.

Ujumbe umekuwa hivi: "Unahimizwa kuja kupiga kura muda huu. Kuna usalama, utulivu na hakuna foleni. Mwambie na mwenzio. Afisa Uchaguzi wa Jimbo."

14:00 Wawafahamu wagombea wote wa urais walio kwenye karatasi za kura visiwani Zanzibar? Kuna wagombea 14. Majina yao ndiyo haya:

1 Khamis Iddi Lila ACT-W
2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA
3 Hamad Rashid Mohamed ADC
4 Said Soud Said AFP
5 Ali Khatib Ali CCK
6 Ali Mohamed Shein CCM
7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA
8 Seif Sharif Hamad CUF
9 Taibu Mussa Juma DM
10 Abdalla Kombo Khamis DP
11 Kassim Bakar Aly JAHAZI
12 Seif Ali Iddi NRA
13 Issa Mohammed Zonga SAU
14 Hafidh Hassan Suleiman TLP

13:00 Mji Mkongwe (Stone Town) ambao ni maarufu sana kwa watalii hauna watu wengi. Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela amepiga picha hizi zinazoonesha mtaa huo ukiwa kama mahame.

Image caption Barabara hazina watu wengi
Image caption Biashara nyingi zimefungwa

11:15 Mwandishi wa BBC Halima Nyanza aliyeko Zanzibar anasema idadi ya watu waliojitokeza katika baadhi ya vituo ni ndogo, tofauti na uchaguzi wa awali Oktoba 25, mwaka jana. Baadhi ya mitaa imeonekana kutulia huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika baadhi ya maeneo.

10:30 Mgombea urais wa chama cha ADC Hamad Rashid amepiga kura yake kituo cha Tondooni Wawi wilaya ya Chake-Chake, mkoa wa Kusini Pemba. Amesema: "Nina imani ya kuwa Rais, nikikosa nitakuwa Makamu wa Rais".

Image caption Bw Rashid akipiga kura

10:00 Mwanamke akitumbukiza kura kwenye kijisanduku kituo cha Kiembe, Samaki. Upigaji kura unaendelea.

08:50 Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein amezungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja.

Mwanzo amezungumzia hatua ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi huo.

Kuhusu amani na utulivu, amesema anaamini kutakuwa na utulivu visiwani.

Hii hapa video yake akizungumza:

Huwezi kusikiliza tena

08:13 Kumbuka, Chama cha Wananchi (CUF) kilitangaza kwamba hakitashiriki uchaguzi wa marudio unaoendelea leo. Chama hicho kinaamini kilishinda uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana na mgombea wake Maalim Seif Hamad anafaa kutangazwa mshindi.

Tume ya uchaguzi Zanzibar hata hivyo ilitangazwa kwamba hakuna aliyejiondoa rasmi kutoka kwa uchaguzi wa leo.

08:00 Maafisa wa usalama wakishika doria mjini Chake kisiwani Pemba.

07:50 Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.

Hapa chini ni tangazo la kuwapasha wateja wa Azam Sealink kwamba hakutakuwa na safari za meli kuanzia tarehe 18 hadi 22 Machi kutokana na uchaguzi unaoendelea Zanzibar.

Licha ya kukatizwa kwa safari, badi wapo watu waliojitokeza wakitarajia kusafiri. Wengi wa waliofika ni wageni kutoka Ulaya ambao hawakuwa na habari.

07:44 Usalama umeimarishwa visiwani. Hapa chini ni maafisa wa usalama wakiwa na mbwa wa kunusa kabla ya Dkt Shein kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Unguja.

07:42 Baadhi ya wapiga kura wakitafuta majina yao kituoni Madungu Chake-Chake, kisiwani Pemba.

07:30 Mwanamke akipakwa wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba.

Baadaye, atabasamu baada kutoka nje ya ukumbi.

07:20 Hii hapa ni picha nyingine ya Dkt Ali Shein, mgombea urais wa CCM baada yake kupiga kura Unguja.

07:05 Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera katika kisiwa cha Unguja.

Image caption Dkt Shein akioneasha wino kwenye kidole chake

07:00 Vituo vingi vya kupigia kura vimefunguliwa.

06:50 Maafisa wa uchaguzi wanajiandaa kufungua vituo. Vituo vinafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri.

06:40 Wapiga kura kituo cha Bungi, Unguja wasubiri kituo kifunguliwe.

06:35 Katika vituo vingi, wapiga kura hajawafika. Lakini maafisa wa tume tayari wamo vituoni pamoja na maafisa wa usalama. Hata ni kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba.

06:30 Hujambo! Wapiga kura visiwani Zanzibar wanashiriki uchaguzi wa marudio leo baada ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba mwaka jana kufutwa na tume ya uchaguzi. Chama cha CUF kinasusia uchaguzi huo.

Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi huo.