Mwandishi akamatwa nchini Uchina

Haki miliki ya picha Apple Daily
Image caption Polisi Beijing

Wakili mmoja aliyekuwa akiliandikia gazeti moja nchini Uchina Jia Jia,ambaye alitoweka wiki iliopita amethibitishwa kukamatwa na maafisa wa polisi wa mji wa Beijing.

Yan Xin amesema kuwa polisi walimuelezea bwana Jia alikamatwa katika uwanja wa ndege wiki iliopita,kabla ya kupanda ndege na kuelekea Hong Kong.

Bwana Jia anadaiwa kuhusishwa na barua inayomtaka rais wa China Xi Jinping kujiuzulu,iliochapishwa katika mtandao mmoja wa serikali mapema mwezi huu.Barua hiyo iliondolewa haraka.

Bwana Yan alichapisha katika mtandao wa WeChat ambao polisi wanasema bwana Jia alishukiwa kuhusishwa katika kesi fulani,lakini hakutoa maelezo.

Marafiki wameviamboa vymbo vya habari kwamba wanaamini bwana Jia alitoweka baada ya kumuonya mhariri rafikiye Ouyang Hongliang,baada ya barua kuchapishwa katika mtandao wa Bwana Ouyang unaojulikana kama Wujie News.

Mtafiti wa shirika la kibinadamu Amnesty International Wiliam Lee Nee ameiambia AFP kwamba kupotea kwa bwana Jia huenda kunahusishwa na barua hiyo.

Amnesty International sasa inataka raia kupigania kuwachiliwa kwa bwan Jia.