Korea Kaskazini yarusha makombora mengine

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maandamano dhidi ya urushaji wa makombora unaofanywa na Korea Kaskazini

Taifa la Korea Kaskazini limerusha makombora kadhaa ya masafa mafupi katika maji ya pwani yake ya mashariki ,kulingana na kituo cha habari cha Korea Kusini Yonhap.

Urushaji wa makombora hayo unajiri siku tatu baada ya Korea Kusini kusema kuwa taifa hilo la Korea Kaskazini lilirusha kombora la masafa marefu baharini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014.

Washington na Seoul zinafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi huku Korea Kaskazini ikidhania inajiandaa kuivamia.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Korea Kaskazini yarusha makombora mengine

Vikwazo vipya dhidi ya taifa hilo vinatokana na hatua ya taifa hilo kuyafanyia majaribio makombora yake ya kinyuklia pamoja na uzinduzi wa kifaa chake cha Satelite mnamo tarehe 7 mwezi Februari ambayo ilikiuka vikwazo vya Umoja wa mataifa vilivyopo.

Korea Kusini ilikuwa ikijaribu kubaini ni aina gani ya makombora yaliohusishwa katika urushaji huo.

Makombora hayo yalidaiwa kurushwa kutoka mji wa Kaskazini Mashariki wa Hamhung.

Siku ya ijumaa Korea Kaskazini ilirusha makombora mawili ya masafa marefu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mokombora ya Korea Kaskazini

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa makombora hayo yaliruka kilomita 800 kabla ya kuanguka majini.

Baadaye Marekani iliitaka Pyongyang kutosababisha wasiwasi.