Rais Obama ziarani Cuba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Barck Obama ziarani Cuba

Rais Barack Obama ameanza ziara ya kihistoria nchini Cuba,hii ikiwa ni ziara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 88 tangu Rais Calvin wa Marekan azuru nchi hiyo mwaka 1928.

Akiwa ameongozana na familia yake Rais Obama alipokelewa na watu wachache tu, mjini Havana huku akikaribishwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bruno Rudriguez.

Hata hivyo amemtembelea askofu wa kanisa Katoliki Jame Ortega ambaye aliwezesha mazungumzo ya siri kati Marekani na Cuba mwaka 2014.

Rais Barack Obama hii leo anatarajiwa kukutana na rais wa Cuba Raul Castro kwa lengo la kuwa na mazungumzo kuhusiana na masuala ya kibiashara na kisiasa.