Qatar 2022: Mashabiki kukita hema jangwani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Qatar 2022: Mashabiki kukita hema jangwani

Waandalizi wa kombe la dunia la mwaka 2022 iliyoratibiwa kufanyika Qatar wamesema, mashabiki watalazimika kukita hema jangwani.

Waandalizi wanakisia kuwa takriban mashabiki nusu milioni watakwenda katika taifa hilo tajiri liliko Ghuba kushabikia timu zao.

Hata hivyo wanasema kuwa kutokana na muda uliosalia na gharama watalazimika kukita hema jangwani ilikuwapa makao maelfu ya mashabiki.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashindano hayo yataandaliwa mwezi wa Desemba kutokana na hofu ya kiwango cha juu cha joto.

Vilevile wanapanga kukodisha meli za kifahari ambazo vilevile zitatia nanga ufukweni ilikuwapa malazi mashabiki zaidi.

''Nguzo moja ya kuu ya kuyaanda mashindano haya Qatar ni kuchochea mtagusano baina ya watu wa matabaka mbalimbali,kwa hivyo ninataka kuwaeleza kuwa kwa kweli tunapanga mikakati ya kuwapa maelfu ya mashabiki fursa ya kulala jangwani na kutizama nyota'' alisema msemaji wa kamati andalizi ya mashindano hayo ya Qatar2022.

Watu wa jamii ya wa Bedoiun walikuwa wakikita hema zao jangwani kwa miaka na mikaka haswa katika safari zao ndefu za kibiashara kati ya jangwa la Syria na Arabia.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandalizi wanakisia kuwa watakuwa na upungufu wa takriban vyumba elfu 60,000.

Hayo sio mabadiliko ya pekee yatakayoshuhudiwa mwaka wa 2022.

Mashindano hayo yataandaliwa mwezi wa Desemba kutokana na hofu ya kiwango cha juu cha joto.

Waandalizi wanakisia kuwa watakuwa na upungufu wa takriban vyumba elfu 60,000.