Twitter yaadhimisha miaka 10 tangu kuanza kutumiwa

Jack Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ujumbe wa kwanza ulitumwa na mwanzilishi mwenza wa Twitter Jack Dorsey

Mtandao wa kijamii wa Twitter unaadhimisha miaka kumi tangu kutumwa kwa ujumbe wa kwanza kabisa.

Ujumbe wa kwanza kwenye mtandao huo ulitumwa na mwanzishili mwenzawa Twitter, Jack Dorsey, akisema: "just setting up my twttr" (ndio tu naanda twttr yangu).

Tangu wakati huo, mtandao wa Twitter umekuwa maarufu sana duniani na kutumiwa sana na wanasiasa, wanaharakati na wanahabari.

Ulichangia sana katika wimbi la mageuzi katika mataifa yaKiarabu na vitambulisha mada vingi vimetumiwa kusisimua hisia za watu.

Image caption Ujumbe wa kwanza wa BBC Swahili katika Twitter

Mfano ni kitambulisha mada ya #jesuisparis baada ya mashambulio ya Paris mwezi Novemba ambapo watu 130 waliuawa.

Wachezaji na wasanii ndio sana huwa na wafuasi wengi zaidi katika Twitter.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Afisa Mkuu Mtendaji wa Twitter Jack Dorsey (kushoto) akiwa na Rais wa Indonesia Joko Widodo makao makuu ya Twitter mjini San Francisco.

Wakati wa kilele chake, kampuni ya Twitter ilikuwa na thamani ya dola 25 bilioni za Marekani.

Lakini thamani ya kampuni hiyo imekuwa ikishuka, na pia imeshutumiwa kutokana na inavyoshughulikia unyanyasaji mtandaoni.