Shein atangazwa mshindi wa urais Zanzibar

Bofya hapa kwa habari za karibuni zaidi

14:30 Dkt Shein, amezungumza na wanahabari kuhusu hatima ya chama cha CUF ambacho kilisusia uchaguzi wa marudio Jumapili. Amesema kwa sasa ataongoza serikali kwa miaka mitano ijayo. Hajafutilia mbali uwezekano wa kufanya kazi na CUF lakini amedokeza kwamba itakuwa vigumu. “Itategemea hali, hawakushiriki uchaguzi hivyo nitafanyaje kazi nao?”

Image caption Wafuasi wa CCM wamesherehekea katika barabara za Unguja

14:00 Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekuwa wakisherehekea katika barabara za mji wa Unguja baada Dkt Ali Mohammed Shein kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio.

Huwezi kusikiliza tena

12:30 Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.

Hamad Rashid Mohamed wa chama cha ADC ndiye wa pili akiwa na kura 9,734.

12:20 Mgombea wa CCM Dkt Ali Mohammed Shein amekabidhiwa cheti wa ushindi wa urais.

12:08 Dkt Ali Mohammed Shein atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar akiwa na kura 299,982.

Huwezi kusikiliza tena

11:57 Mgombea urais wa CCM Dkt Ali Mohammed Shein yumo ukumbini.

11:54 Bw Jecha kwa sasa anatoa hotuba ya kufungua kikao cha kutangazwa kwa matokeo.

11:49 Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha amewasili ukumbi wa kutangaziwa matokeo. Tume imesema itatangaza matokeo yote muda mfupi ujao.

11:27 Gazeti la Mwananchi linaripoti kwamba mgombea urais wa CCM Dkt Ali Mohamed Shein aongoza matokeo ya awali ya urais majimbo ya Chonga kura 3598, Ziwani (2890), Wawi (4147), Ole (3818), Chake Chake (4551). Matokeo rasmi bado yanasubiriwa.

11:00 Baadhi ya waliowania urais wamefika ukumbini na kuketi. Mmoja wao ni mgombea wa ADC Hamad Rashid.

10:30 Wanahabari, waangalizi na maafisa wengine wa uchaguzi tayari wamo ukumbini wakisubiri kuanza kutangazwa kwa matokeo.

10:20 Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua rais. Majina yao ndiyo haya:

1 Khamis Iddi Lila ACT-W
2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA
3 Hamad Rashid Mohamed ADC
4 Said Soud Said AFP
5 Ali Khatib Ali CCK
6 Ali Mohamed Shein CCM
7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA
8 Seif Sharif Hamad CUF
9 Taibu Mussa Juma DM
10 Abdalla Kombo Khamis DP
11 Kassim Bakar Aly JAHAZI
12 Seif Ali Iddi NRA
13 Issa Mohammed Zonga SAU
14 Hafidh Hassan Suleiman TLP

10:15 Ulinzi mkali umewekwa katika ukumbi wa kutangazia matokeo. Mbwa wa ulinzi pia wametumika kukagua eneo hilo, ambalo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Selim Jecha Selim anatarajiwa kutumia kutangaza matokeo.

10:00 (Saa za Afrika Mashariki). Hujambo! Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa marudio uliofanyika visiwani Zanzibar Jumapili yanatarajiwa kutangazwa leo.

Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu kutangazwa kwa matokeo hayo.