Apple yazindua iPhone na iPad Pro ndogo

Haki miliki ya picha Apple
Image caption Iphone

Kampuni ya Apple imetangaza uzinduzi wa simu ndogo aina ya iPhone pamoja na iPad katika sherehe iliofanyika mjini San Fransisco na kupeperushwa moja kwa moja mtandaoni.

Simu hiyo kwa jina iPhone SE ina utendakazi sawa na simu ya Apple 6s,na ina uwezo wa kuchukua video za 4k.

Nayo IPad Pro ina kioo chenye ukubwa wa nchi 9.7 ikiwa ni sawa na iPad ile ya zamani.

Haki miliki ya picha Apple
Image caption Simu za Apple

Simu hiyo mpya itapatikana katika mataifa 110 kufikia mwishoni mwa mwezi Mei.

Ikiwa na bei ya kati ya dola 399 na 499,simu hiyo ndio ya bei rahisi kuwahi kutolewa na kampuni ya Apple ,imesema Apple.

Pia imesema kuwa iPad Pro itapatikana katika aina tatu za ukubwa huku kukiwa na ile yenye ukubwa wa zaidi ya 256GB.

Bei yake itaanzia dola 599 kwa ile ndogo na itapatikana nchin Marekani mwishoni mwa mwezi huu.

Haki miliki ya picha Apple
Image caption ipad pro

Apple imesema kuwa iliuza simu milioni 30 zenye ukubwa wa nchi 4 mwaka uliopita ,hatahivyo mauzo yake ya simu yamepungua katika miezi ya hivi karibuni kulingana na soko la simu aina ya smartphone.