Mambo muhimu kuhusu milipuko Brussels

Zaventem Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uharibifu uliosababishwa na milipuko uwanja wa ndege wa Zaventem

Mashambulio kadha yametekelezwa katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels na kusababisha vifo vya watu takriban 13.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wasafiri waliokwama uwanja wa ndege

Haya hapa ni maelezo muhimu kuhusu mashambulio hayo.

 • Kulitokea milipuko miwili katika uwanja wa ndege wa Zaventem mwendo wa saa nne asubuhi saa za Afrika Mashariki watu waliokuwa wakitaka kuondoka walipokuwa kwenye foleni.
 • Waziri wa afya wa Ubelgiji amesema watu 11 walifariki na wengine 81 kujeruhiwa baada ya milipuko miwili kutokea uwanja wa ndege wa Zaventem, nje kidogo ya mji wa Brussels.

  Meya wa Brussels amesema watu 20 walifariki Maelbeek.

 • Kundi linalojiita Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo.
 • Milio ya risasi ilisikika kabla ya milipuko hiyo, ambayo inaonekana kuwa ilitokea karibu na meza za mashirika ya ndege ya American Airlines na Brussels Airline.
 • Muda mfupi baadaye, karibu saa moja hivi, mlipuko ulitokea katika kituo cha treni cha Maalbeek, karibu na majengo ya Umoja wa Ulaya.
 • Serikali ya Ubelgiji imepandisha kiwango cha tahadhari hadi alama 4, kiwango cha juu zaidi.
 • Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ametangaza kwamba ataandaa kikao cha kamati ya serikali inayoshughulikia dharura.
 • Safari za ndege kuingia na kutoka uwanja wa Zaventem zimesitishwa, sawa na uchukuzi wa treni Brussels .
 • Haki miliki ya picha AP
  Image caption Maafisa wa matibabu wakihudumia watu waliojeruhiwa
 • Ulinzi umeimarishwa katika uwanja wa ndege wa Gatwick, jijini London.
 • Taasisi za Umoja wa Ulaya zimefutilia mbali mikutano yote mjini Brussels. Wanaoruhusiwa kuingia majengo ya umoja huo ni wafanyakazi pekee walio na vitambulisho.
 • Kituo cha televisheni cha RTBF kimemnukuu mwendesha mashtaka wa serikali Ubelgiji akisema shambulio la uwanja wa ndege wa Zaventem lilikuwa la kujitoa mhanga.