Burundi: Mkuu wa jeshi auawa kambini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Burundi: Mkuu wa jeshi auawa kambini

Afisa mmoja muandamizi wa jeshi la Burundi ameuwawa leo ndani ya makao makuu ya jeshi la Burundi.

Kanali Darius Ikurakure alikuwa Kamanda wa kambi ya kijeshi ya Muzinga, nje kidogo ya jiji la Bujumbura.

Kambi ya Muzinda iko kilomita 30 kutoka mji mkuu wa Bujumbura.

Haki miliki ya picha ap
Image caption Kanali Ikurakure alikua msatari wa mbele katika harakati za kuzima maandamano na ghasia dhidi ya rais Pierre Nkurunziza

Kanali Ikurakure alikua msatari wa mbele katika harakati za kuzima maandamano na ghasia zilizotokea baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu mamlakani.

Duru kutoka kwa jeshi la burundi zinasema kuwa kanali huyo alipigwa risasi na mwanajeshi mwenza.