''Karibu niwe mlipuaji wa kujitoa mhanga''

Image caption Mlipuaji wa kujitolea muhanga katika kundi la Boko Haram Nigeria

Siku ya Jumanne tarehe 9 mwezi wa Februari ,wasichana 2 wa Nigeria waliingia katika kambi moja ya watu waliowachwa bila makao Kaskazini mashariki mwa taifa hilo.

Dakika chache baadaye walijilipua na kuwaua watu 58.

Msichana wa tatu alikataa kushiriki katika shambulio hilo la Boko Haram na hii ni habari yake.

Huawa sio jina lake,hajui umri wake lakini anaonekana kuwa na kati ya miaka 17 na 18.

Alikamatwa na kundi la Boko haram kwa zaidi ya mwaka mmoja wakati watekaji wake walipopanga kushambulia kambi ya Dikwa.

Haki miliki ya picha
Image caption Bomu la mlipuaji wa kujitolea muhanga

Badala ya kushiriki katika shambulo la kujitolea muhanga,wasichana hao waliambiwa kwamba watakwenda moja kwa moja peponi.

Lakini Hauwa alikataa.Nilisema sitaki kwa kuwa mamaangu anaishi Dikwa,sitakwenda kuwauwa watu huko.

Badala yake ningependa kwenda kuishi na familia yangu hata iwapo nitakufa nikiwa huko,aliniambia kupitia mkalimani.

Wazazi wake wote na nduguze,isipokuwa kakaake moja ambaye alikuwa ametekwa pamoja naye walikuwa wakiishi katika kambi ya Dikwa katika jimbo la Borno,pamoja na wengine 50,000 waliotekwa kwa lazima katika makaazi yao.

Hauwa anaelezea vile alivyoshawishiwa kujiunga na kundi hilo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Milli ya watu waliouawa kufuatia shambulio la kujitolea muhanga nchini Nigeria

''Nilikuwa na matatizo ya kiroho kwa hivyo Boko haramu liliniambia watanisaidia kukabiliana nayo'',alisema.

Hatujui kile Hauwa alichokuwa akiugua,lakini mapepo hayo yalimfanya ajimwagie mchanga na hata kujichoma mkono wake.

Hivyobasi aliona Kundi la Boko haram kama jibu la matatizo yake na hivyobasi wakamchukua.

Anakumbuka siku moja akiishi na wapiganaji hao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ulipuaji wa kujitolea muhanga NIgeria

''Tulikuwa tukiishi katika nyumba ya nyasi .wakati mume wangu alipokuwa ,nilipika mara tatu kwa siku ,wanaume walikuwa wakiiba nyama na kutuletea tupike''.

Baada ya mda fulani,Hauwa aliwachana na mumewe na akaolewa tena.

Mumewe wa pili alitoroka na alipokataa kuolewa na mume wa tatu kundi hilo lilipendekeza mpango wake.

''Walisema kwamba kwa sababu nimekataa kuolewa tena,nijilipue na bomu'',alisema.

Kambi hiyo ya Dikwa ya wakimbizi wa ndani kwa ndani ilikuwa kilomita 85 kaskazini mashariki mwa mji wa Maiduguri,mji mkuu wa jimbo la Borno na chimbuko la kundi la Boko Haram.

Hauwa aliijua kambi hiyo na alijua pia kwamba sio mbali na eneo analozuiliwa na wapiganaji hao,kwa hivyo usiku kabla ya shambulio hilo kufanyika alitoroka mapema asubuhi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Shambulio la kujitolea muhanga Nigeria

Mpango wake ulikuwa kuijuza familia yake na watu wengine wanaoishi Dikwa kuhusu shambulio hilo.

Alipokuwa karibu kufika katika kambi ya Dikwa wapiganaji wawili wa kujitolea muhanga walijilipua.

Afisa mmoja wa jeshi aliionyesha timu ya BBC eneo la shambulio hilo.

Mwanamke mmoja Falmata Mohammed anakumbuka dakika chache kabla ya shambulio.

Mwanajeshi mmoja alikuwa akijaribu kupanga foleni,na kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye alikuwa amevalia kilemba chekundu na alikuwa na nywele ndefu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waathiriwa wa shambulio la kujitolea muhanga nchini Nigeria

Lakini alikuwa amechelewa.Falmata anasema kuwa aliangalia kila upande wakati mwanamke mmoja alipoanza kulalamika kuhusu wanajeshi waliokuwa wakiwatawanya watu.

Tulipokuwa tukielekea alipiga kelele 'Wayyo',akisema alikuwa na uchungu tumboni....watu walikimbia kumsaidia na kujaribu kumbeba na ni wakati huo ambapo bomu hilo lililipuka.

Tuliona cheche za moto ,aliniambia,akisema kwamba alizingirwa na vipande vya miili.

Hauwa hakuliona shambulio hilo yeye mwenyewe lakini alionyeshwa picha za baada ya shambulio hilo na wanajeshi na kuona hatma ya wasichana hao wawili waliojitolea muhanga.