Kundi la Al-Qaeda lakiri kushambulia hoteli Mali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya raia walionusuriwa

Tawi la kundi la wapiganaji wa Al-Qaeda kaskazini mwa Afrika Islam Maghreb AQIM limesema kuwa lilitekeleza shambulio katika hoteli moja mjini Bamako nchini Mali ambayo ilikuwa makao makuu ya ujumbe wa mafunzo ya Muungano wa Ulaya.

Kundi hilo lilitoa madai hayo katika mtandao wa kijamii lakini halikutoa maelezo yoyote.

Wapiganaji wawili waliishambulia hoteli hiyo ya Nord-Sud Azalai siku ya Jumatatu jioni.

Shambulio hilo lilitibuliwa na mmoja ya wapiganaji hao kuuawa ,ijapokuwa haijulikani iwpo mpiganaji wa pili alitoroka.

Ujumbe wa Muungano wa Ulaya umesema kuwa hakukuwa na majeruhi yoyote miongoni mwa wafanyikazi wake.

Makumi ya watu waliuawa katika shambulio la AQIM mnamo mwezi Novemba katika hoteli ya Radisson Blu hoteli mjini Bamako.

Shambulio hilo linajiri wiki moja baada ya wapiganaji kuwapiga risasi watu 18 katika hoteli moja ilio ufukweni wa bahari nchini Ivory Coast.