Suu Kyi kuteuliwa waziri Myanmar

Suu Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jina la Suu Kyi limewasilishwa kwa bunge

Kiongozi mtetezi wa demokrasia nchini Myanmar Aung San Suu Kyi ambaye chama chake kilishinda uchaguzi mkuu Novemba mwaka jana atateuliwa kuwa waziri.

Jina la Suu Kyi lilikuwa kwenye orodha ya watu watakaoteuliwa mawaziri ambayo iliwasilishwa na chama chake National League for Democracy na kusomwa na spika wa bunge.

Atakuwa waziri katika afisi ya rais na atasimamia wizara nne: wizara ya masuala ya kigeni, wizara ya elimu, wizara ya stima na wizara ya kawi.

Htin Kyaw ndio rais mpya wa Myanmar

Viongozi wa zamani wa kijeshi nchini Myanmar, ambayo zamani ilifahamika kama Burma, waliingiza kifungu kwenye katiba ya nchi hiyo ambacho kinamzuia kuwa rais kwa sababu wanawe wawili wana pasipoti za Uingereza.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Htin Kyaw akiwa na Suu Kyi mwaka 2010

Mshirika wake mkuu Htin Kyaw alichaguliwa kuwa kiongozi wan chi hiyo wiki iliyopita.

Kabla ya uchaguzi, Suu Kyi alikuwa amedokeza kwamba atashiriki katika uongozi wa nchi hiyo na kusema atakuwa "juu ya rais”.