Virusi vya Zika vyafika Korea Kusini

Zika Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Virusi vya Zika vinaenezwa sana na mbu

Korea Kusini imethibitisha kwamba mwanamume mmoja raia wa nchi hiyo aliyekuwa amezuru Brazil ameambukizwa virusi vya Zika.

Mwanamume huyo alirejea nchini Korea Kusini majuzi.

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Maradhi cha nchi hiyo kimesema mwanamume huyo wa umri wa miaka 43 aligunduliwa kuwa na virusi hivyo Jumanne na anatibiwa mjini Gwangju.

Virusi vya Zika huenezwa sana na mbu na vilitangazwa kuwa dharura ya kimataifa duniani na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Haki miliki ya picha AP
Image caption Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo

Virusi hivyo vinaenea kwa kazi Brazil nan chi nyingine za Marekani na unaaminika kusababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo.

Visa kadha vya maambukizi vimeripotiwa barani Asia.

Haki miliki ya picha Reuters

Korea Kusini imesema mwanamume huyo ametengwa na wanafuatilia maeneo yote aliyopitia na watu aliokutana nao tangu kurejea nyumbani, shirika la habari la Yonhap limesema.