Al Shabab yapiga marufuku bidhaa za Uturuki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Al Shabab yapiga marufuku bidhaa za Uturuki

Kundi la wanamgambo wa Al Shabab limepiga marufuku uuzaji na ununuzi wa bidhaa zilizoundwa Uturuki nchini Somalia.

Al-Shabab imewaarifu wafanyibiashara katika majimbo ya Kusini mwa Somalia na maeneo ya Lower Shabelle kuwa bidhaa zinazotokea Uturuku ni haramu.

Jarida linalochapishwa kwenye tovuti ya Falaar inasema kuwa wale watakaokiuka amri hiyo ''watachomwa moto wakiwa hai''

Wafanyibiashara katika maeneo yaliyoathirika tayari wamelalamika kuwa amri hiyo itawaathiri vibaya.

Al-Shabab inasema kuwa imechukua hatua hiyo kwani Uturuki inasaidia mahasidi wao serikali ya Somalia.

Haki miliki ya picha
Image caption Wafanyibiashara kutoka Uturuki wamewekeza katika biashara nyingi nchini Somalia na haswa Mogadishu.

Hii sio mara ya kwanza kwa Al shabab kuilenga Uturuki.

Awali Al Shabab ilikuwa imelalamika kuwa bidhaa zinazotokea Uturuki zinatokomeza uchumi wa Somalia.

Wafanyibiashara kutoka Uturuki wamewekeza katika biashara nyingi nchini Somalia na haswa Mogadishu.