UN: Watu 474 wameuawa Burundi

Rais Pierre Nkurunziza Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ghasia za mauaji zilianza baada ya rais Pierre Nkurunziza pichani kutangaza nia yake ya kuwania muhula watatu

Takwimu mpya kutoka Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa watu 474 wamekwishauawa nchini Burundi tangu mwezi Aprili mwaka jana, wakati mzozo ulipoibuka kufuatia uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu madarakani.

Wataalam watoa matokeo ya uchunguzi kutokana na ziara waliyoifanya nchini Burund mapema mwezi huu mbele ya Braza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Haki miliki ya picha
Image caption Serikali ya Burundi inasema mauaji yalitekelezwa na waasi

Lakini kiongozi wa shirika la haki za binadamu la Burundi amesema kuwa idadi ya waliouawa inazidi watu 600.

Muakilishi wa serikali ya Burundia amesema kuwa mauji yalitekelezwa na waasi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mauji dhidi ya viongozi wa kijeshi yamekua yakitekelezwa kwenye maeneo ya mji wa Bujumbura

Jumanne, afisa wa ngazi ya juu wa kijeshi na mshirika wa rais alipigwa risasi na kuuawa kwenye ofisi ya wizara ya ulinzi.

Meja mwingine ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa usiku wa kuamkia leo alipokua akiondoka kwenye baa katikati mwa mji mkuu, Bujumbura.