ICC yamfungulia Ongwen LRA mashtaka 70

Image caption ICC yamfungulia Ongwen LRA mashtaka 70

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita yenye makao yake makuu mjini Hague Uholanzi imemfungulia mashtaka 70 kiongozi wa kundi la waasi wa The Lords Resistance Army LRA , Dominic Ongwen.

Mahakama hiyo imemfungulia mashtaka ya uhalifu wa kivita, ubakaji,mauaji ya halaiki,utumizi wa wafungwa wa ngonomiongoni mwa makosa mengi.

Ongwen ndiye kamanda wa kwanza wa kundi hilo la LRA kushtakiwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ongwen ndiye kamanda wa kwanza wa kundi hilo la LRA kushtakiwa.

Ongwen ambaye anatambuliwa kwa jina la utani la 'White Ant' alitekwa akiwa bado mtoto na wapiganaji wa LRA kabla ya kukuwa moja kati ya makamanda wakuu wa waasi hao ambao wanapigania kuvunjwa kwa serikali ya Yoweri Museveni na badala yake kuundwe serikali inayotii amri kumi za mungu.

Kundi hilo la waasi lilianzia Uganda na kuenea Sudan Kusini Chad na hata Afrika ya Kati.

Waasi hao wa LRA wametuhumiwa kwa kuwateka watoto na wanawake kukata mapua na masikio wahanga wake.