Wakimbizi wamuokoa mwanasiasa Ujerumani

ajali ya gari Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi walimpatia huduma yakwanza mwanasiasa wa NDP kabla ya polisi kuwasili kwenye eneo la ajali

Mwanasiasa kutoka chama cha mrengo wa kulia cha Ujerumani ameokolewa baada na wakimbizi baada ya gari lake kugonga mti, zimeeleza ripoti za vyombo vya habari vya Ujerumani.

Raia wawili wa Syria walitoa huduma ya kwanza kwa mwasiasa huyo wa chama cha National Democratic Party (NPD) Stefan Jagsch ambae aliejeruhiwakatika ajali katika jimbo la Hesse , liliarifu shirika la habari la DPA.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wafuasi wa chama cha NPD wamekua wakishiriki maandamano ya kupinga wahamiaji

Inasemekana wakimbizi hao waliokua wakipita karibu na ajali hiyo walikua wameondoka polisi walipowasili kwenmye tukio.

Wanasiasa wa chama hicho cha NPD wamekua wakishiriki katika mfulurizo wa maandamano ya kupinga wahamiaji nchini Ujerumani.

Hata hivyo afisa wa kikanda wa NPD Jean Christoph Fiedler aliwasifu wakimbizi hao wawili kwa ''kitendo hicho kizuri sana cha kibinadamu'', liliripoti gazeti la Frankfurter Rundschau.

Mahakama ya katiba ya Ujerumani kwa sasa inaangalia uwezekano wa kupiga marufuku chaka cha NPD juu ya madai kwamba kina itikadi za ubaguzi.