Magaidi tishio Ulaya:Carter

Image caption Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter

Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter amesema shambulio lililofanyika dhidi ya Ubeligiji linabainisha wazi kwamba nchi za Ulaya zinatakiwa kuongeza kasi ya kutokomeza ugaidi.

Amesema kuwa makundi ya wapiganaji wa Kiislam nchini Syria na Iraq moja ya tishio kwa nchi ya Ulaya na kwamba yakiachwa yaendelee kustawi yatazitesa nchi za Ulaya

Carter amesema nchi za Ulaya kuchangia jitihada za kuwakabili makundi hao kama ambavyo Marekani imekuwa ikifanya.

Awali rais Obama amesema kuangamiza makundi haya ya kigaidi ilikuwa ndiyo kipaumbele chake cha kwanza wakati akipokuwa akiingi madarakani. Amesema pia itakuwa ni kosa kujitenga na jumuiya za kiislam nchini Marekani