Boko Haram watoa kanda mpya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram watoa kanda mpya

Kinara mkuu wa kundi la wapiganaji la Boko Haram nchini Nigeria, ameonekana katika mkanda wa video uliowekwa mtandaoni.

Kwa mara ya kwanza baada ya kimya cha mwaka mmoja hivi, Abubakar Shekau,ameonekana akiwa amevalia magwanda ya kijeshi lakini bila ujasiri wake wa kawaida.

Shekau amekuwa mafichoni baada ya kundi lake kuvamiwa na majeshi ya muungano wa kanda ya Afrika Magharibi.

Kiongozi huyo wa Boko Haram anawashukuru wapiganaji wake ambao anasema wamekuwa ni wajasiri mno, ishara ya kukabiliwa na upinzani mkali wa majeshi ya Muungano wa Mataifa ya Magharibi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shekau amekuwa mafichoni baada ya kundi lake kuvamiwa na majeshi ya muungano wa kanda ya Afrika Magharibi.

Kundi hilo limekabiliwa vikali na majeshi ya Nigeria baada ya rais mpya wa nchi hiyo Muhamadu Buhari kutangaza vita kwa nia ya kuitokomeza kabisa jeshi hilo.

Boko Haram imesababisha vifo vya maelfu ya wakaazi wa Nigeria na mataifa wanachama wa muungano unaopambana nao mbali na kusababisha mamilioni ya watu Magharibi mwa Afrika hasa kaskazini mwa Nigeria kutoroka makwao.

Kampeini ya muungano huo umekomboa miji yote iliyokuwa imekaliwa na kundi hilo la Boko Haram.

Haki miliki ya picha b
Image caption Mungano huo unajumuisha majeshi ya Nigeria Cameroon na Chad.

Mungano huo unajumuisha majeshi ya Nigeria Cameroon na Chad.

Tangu mwaka wa 2009 kundi hilo linalaumiwa kwa vifo vya watu takriban 20,000.