Ghana yanasa askari wa Afrika Kusini

Image caption BNI inasema kuwa watatu hao walikamatwa pamoja na vijana 15 walokuwa wanafunzwa

Maafisa watatu wa polisi wa zamani wa Afrika Kusini wamekamatwa nchini Ghana kwa makosa ya kufunza vijana mbinu za kutumia silaha kinyume cha sheria na kwa kupanga njama ya kutekeleza maasi nchini humo.

Vilevile Maafisa hao wa polisi wa zamani wanakabiliwa na makosa ya kudanganya.

Idara ya upelelezi nchini humo (The Bureau of National Investigation ;BNI) liliwakamata watuhumiwa hao katikati ya nchi baada ya kupata ujasusi kuwa kulikuwepo na kambi haramu eneo hilo.

Image caption Ghana yanasa askari wa Afrika Kusini

BNI inasema kuwa watatu hao walikuwa wanahatarisha usalama wa Ghana.

BNI inasema kuwa watatu hao walikamatwa pamoja na vijana 15 walokuwa wanajifunza mbinu za kukabiliana na adui wakiwa wamejihami na pia bila ya kuwa na silaha.

Haki miliki ya picha Chris Stein AFP
Image caption BNI inasema kuwa watatu hao walikuwa wanahatarisha usalama wa Ghana.

Aidha walikuwa wamewafunza mbinu za kutumia silaha.

Idara hiyo ya upelelezi inasema kuwa wakati huu ambao kumetokea mashambulizi katika kanda ya hiyo ya Afrika Magharibi , kuwepo kwao nchini Ghana ni tishio la usalama.

Kundi hilo yamkini lilitetwa nchini Ghana na Chama cha New Patriotic ilikuwafunza mbinu za kutoa ulinzi kwa viongozi wa chama hicho huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi Novemba.