ICC: Radovan Karad-žic afungwa miaka 40 jela

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ICC: Radovan Karad-žic afungwa miaka 40 jela

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai -ICC, ya huko The Hague nchini Uholanzi, imemhukumu jela miaka 40, kiongozi wa zamani wa Bosnia/ Serbia, Radovan Karad-žic.

Rais huyo wa zamani amehukumiwa kwa kuhusika na uhalifu wa kivita , pale alipowalenga, raia wengi wao jamii ya kiislamu, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sarajevo miaka ya tisini.

Jaji wa mahakama ya ICC O-Gon Kwon, alisema kuwa Bwana Karad-zic, alihusika moja kwa moja katika mauwaji dhidi ya halaiki mbali na uhalifu mwingine:

"Hatimaye, katika mahusiano ya eneo la manispaa ya matukio hayo, kwa mjibu wa kifungu cha 71 cha mahakama ya jinai, mshtakiwa moja kwa moja anapatikana na makosa ya kuhusika na uhalifu, kutesa, kuangamiza, kuuwa, kuwabeba, kuwahamisha kwa nguvu na ukiukaji wa sheria za kivita.''

''Aidha, ili kukamilisha hukumu hii, mahakama hii bado haijakubali kwamba mshtakiwa hakuelewa wala kuhusika na mauwaji ya halaiki yaliyotokea katika manispaa saba ya mji huo kulingana na kesi ya kwanza ya mauwaji ya halaiki."Jaji O-Gon Kwon alisoma hukumu hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zaidi ya watu 180,000 walifariki katika mapigano yaliyoendelea kwa miaka mitatu u nusu.

Bwana Karadzic, amekiri makosa hayo ya kivita lakini amekanusha kuhusika moja kwa moja.

Zaidi ya watu elfu 180, waliuwawa wakati wa vita hivyo, uliochangia kuvunjika kwa muundano wa Usovieti mbali na kujitenga na jimbo la Yugoslavia na kuwa taifa huru.

Kiongozi huyo wa zamani wa Serbia, Radovan Karaddzic alikuwa anakabiliwa na mashtaka mengi ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu, yaliyotekelezwa wakati wa vita vya Bosnia vya mwaka wa 1990.

Zaidi ya watu 180,000 walifariki katika mapigano yaliyoendelea kwa miaka mitatu u nusu.

Bwana Karadzic alikuwa anatuhumiwa kwa kuwa na maongozi ya kulenga nyumba za watu ambao si Waserbia, ambapo aliwatimua kutoka nyumbani kwake na kuwapeleka sehemu walikouliwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Zaidi ya Waislamu 30,000 waliuawa katika mapigano hayo.

Zaidi ya Waislamu 30,000 waliuawa katika mapigano hayo.

Bwana Karadzich anakiri kuwa uhalifu ulitekelezwa wakati wa vita hivyo lakini akakanusha kuwa yeye aliwajibika na vitendo vya watu walioshuriki.

Alisema vitendo hivyo vya uhalifu vilifanywa lakini havikushirikisha wanajeshi wake.

Ni hukumu ya makosa ya kivita inayotarajiwa na wengi, tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili.