20 Wakamatwa kwa barua ya kumtaka Xi Jinping ajiuzulu

Haki miliki ya picha Apple Daily
Image caption Mwandishi Jia Jia anayehusishwa na barua inayomtaka Xi Jinping ajiuzulu

Takriban watu 20 wamekamatwa nchini Uchina kufuatia uchapshaji wa barua inayomtaka rais Xi Jinping kujiuzulu,BBC imebaini.

Barua hiyo ilichapishwa mapema mwezi huu katika mtandao mmoja wa serikali kwa jina Wujie News.

Licha ya kuondolewa haraka na serikali,maelezo mengine ya barua hiyo bado yapo katika mtandao.

Barua hiyo iliandikwa hivi:

''Kwa rafiki yangu Xi Jinping,sisi ni wanachama shupavu wa chama cha kikomyunisti'',Inaanza.

''Tunaandika barua hii tukikuomba ujiuzulu katika nyadhfa zote za chama na zile za serikali''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Xi Jinping

Lakini nchini Uchina na hususan katika mtandao ulio rasmi,kitendo kama hicho hakijawahi kutokea na tayari kumekuwa na hatua kali zinazochukuliwa na serikali.

Kukamatwa kwa mwandishi maarufu wa gazeti Jia Jia kunahusishwa pakubwa na barua hiyo.

Marafiki ze wanasema alimpigia simu muhariri wa Wujie ili kuweza kupewa habari kuihusu baada ya kuiona mtandaoni.