Marekani na Urusi wasaka amani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, amesema kuwa amekubaliana na Urusi juu ya kuimarisha mashauriano ya amani ya kupata suluhu ya mpito ya kisiasa nchini humo.

Amesema hayo baada ya kukutana na Rais Putin jijini Moscow.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi, Sergey Lavrov, alisema kuwa nchi yake na Marekani itahimiza Serikali na Makundi ya Upinzani wafanye mashauriano.