Video za Justin Bieber zatazamwa mara bilioni 10

Haki miliki ya picha AP
Image caption Justin Bieber

Mwanamuziki Justin Bieber amevunja rekodi ya Vevo kwa video yake kutazamwa mara bilioni 10.

Msanii huyo wa Canada ambaye alitoa kibao kipya Purpose in Novemba alipata idadi hiyo katika kipindi cha miaka sita na miezi mitatu au siku 2,316.

Kutazamwa kwa video zake mara bilioni 4 kulifanyika baada ya Septemba mwaka jana na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa katika kilele cha chati ya muziki katika Vevo kwa wiki 19 mfululizo.

Justin Bieber,Katy Perry na Taylor Swift ni wasanii pekee wenye video mbili tofauti zilizotazamwa zaidi ya mara bilioni moja kila moja.

Image caption Katy Perry

Lakini video yake ya What Do You Mean?Itafikisha kutazamwa mara bilioni moja katika kipindi cha wiki chache zijazo,na kumfanya kuwa msanii wa kwanza kuwa na video tatu zilizotazamwa mara bilioni moja.

Mnamo mwezi Januari ,David Bowie alivunja rekodi ya Vevo kwa siku moja.

Video zake ziliangaliwa mara milioni 51 baada ya kutangazwa kwamba amefariki akiwa na umri wa miak 69.