Wanawake 16 watekwa nyara na Boko Haram Nigeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wapiganaji wa Boko Haram

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamewateka nyara wanawake 16 katika eneo la mashambani kaskazini mashariki mwa jimbo la Adamawa huko Sabon Garin Madagali.

Wakaazi wanasema kuwa wanawake hao walitekwa msituni walipokuwa wakitafuta kuni na kuvua samaki katika mto chini ya ulinzi wa vijana wawili wa kuweka usalama wanaolisaidia jeshi dhidi ya wapiganaji hao.