Adele aomba msamaha baada ya shabiki kujeruhiwa

Image caption Adele

Mwanamuziki wa muziki wa Pop Adele ameomba msamaha baada ya shabiki mmoja kujeruhiwa alipoangukiwa na nyororo katika tamasha la Glasgow.

Nyota huyo alikuwa anaendelea na onyesho lake katika ukumbi wa SSE Hydro siku ya ijumaa usiku wakati nyororo hiyo ilipomuangukia mwanamke huyo aliyekuwa amekaa katika eneo la mashabiki.

Alichukuliwa na kupelekwa hospitali kama tahadhari kulingana na msemaji wa ukumbi huo.

Adele baadaye alituma ujumbe katika mtandao wake wa Tweeter akisema: Pole kwa kusikia kwamba kuna mtu alijeruhiwa katika tamasha yangu usiku.

Uchunguzi unaendelea ili kuhakikisha kisa kama hicho hakitokei tena.