Rais kuongoza kwa muhula mmoja Benin

Image caption Rais Patrice Talon

Rais mpya aliyechaguliwa nchini Benin, Patrice Talon, anasema anataka kupunguza muda wa rais anaoweza kuongoza, kuwa muhula mmoja tu wa miaka mitano.

Bwana Talon, ambaye alimshinda waziri mkuu katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais juma lilopita...amesema muda mfupi wa uongozi utasaidia kile alichoelezea kuwa rais kuridhika na kutokuwa na hima akiongoza muda mrefu.

Alisema atakuwa na mawaziri 16, karibu nusu tu ya idadi ya zamani.

Rais anayestaafu, Thomas Boni Yayi, ametumikia mihula miwili.

Msimamo wa rais mpya wa Benin ni tofauti na viongozi wengine wa Afrika, ambao hivi karibuni wameongeza muda wao wa uongozi.