UN: Dhulma za kingono dhidi ya raia CAR zaendelea

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa

Ubalozi wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati , CAR, umesema kuwa umepokea habari kuhusu udhalilishaji wa kingono unaotekelezwa na wanajeshi na maafisa wa Umoja huo miongoni mwa raia.

Kulingana na taarifa hizo udhalilishaji huo ulifanywa kati ya mwaka wa 2014 na 2015 katika eneo la Kati mwa Kemo.

Umoja wa Mataifa ulisema kuwa utachunguza madai hayo.

Image caption Mwanajeshi wa Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa katika CAR umekumbwa na malalamishi na kashfa nyingi zinazohusu ngono miongoni mwa wanajeshi na wafanyakazi wake.

Majuma mawili yaliyopita azimio lilipitishwa ili Muungano huo uwarejeshe nyumbani wanajeshi wake wote iwapo watakabiliwa na lawama za makosa ya kingono tena.