Sanders apania kupunguza uongozi wa Clinton US

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bernie Sanders apania kupunguza uongozi wa Clinton

Mbombea wa urais nchini Marekani kupitia tiketi ya chama cha Democrat Bernie Sanders atajaribu kupunguza uongozi wa Hillary Clinton katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa mgombea wa chama cha Democrat siku ya Jumamosi katika kura za Hawaii na Alaska katika jimbo la Washington.

Bwana Sanders bado hajakata tamaa lakini Hillary tayari amejishindia wajumbe 1691 kati ya wajumbe 2,383 wanaohitajika kushinda.

Bado anaendelea kuvutia makumi ya maelfu katika mikutano yake ya kampeni huku akiitisha mageuzi ya kisiasa .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bernie Sanders

Bi Clinton amesema kuwa ana kura milioni 2.6 zaidi ya Sanders.Kura ya Jumamosi ni ya wagombea wa chama cha Demokrat pekee .

Bwana Sanders ametumia wiki yote akiwa magharibi mwa pwani akitafuta uungwaji mkono miongoni wale wanaounga mkono mabadiliko na wale wa mrengo wa kushoto.